Journal of Swahili Studies https://journals.pu.ac.ke/index.php/jss
Journal of Kiswahili Studies (JSS) ni jarida lenye matoleo mawili kwa mwaka lililoanzishwa kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Pwani na TUSIMA (RISSEA), na kufadhiliwa na Prof. Rajab, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Pwani. Jarida hili lilianzishwa kwa minajili ya kukuza na kuendeleza utafiti na utaalamu wa lugha ya Kiswahili kwa kuwapatia watafiti wa taaluma mbalimbali, hasa za lugha ya Kiswahili, Fasihi na Utamaduni, nafasi ya kuchapisha matokeo ya tafiti zao.
JSS, ni jarida ambalo makala yake hudurusiwa kwa uhakiki na uhariri wa upofu ili kuhakikisha uzito wa kiakademia wa makala unadumishwa. Ni matumaini ya Mhariri kwamba wasomi wa majarida yetu watanufaika mno kwa elimu iliyomo katika makala ya jarida hili na vile vile ni matumaini yetu kwamba watafiti wengi wengine watahamasika kwa kusoma majarida yetu na kutuma makala ya tafiti zao ili yachapishwe.
Ijapo kwa sasa jarida hili linachapisha makala ya Kiswahili, Fasihi na Utamaduni hatutasita kufungua milango ya makala ya taaluma nyengine za kisayansi, kiteknolojia na kielimu kwa Kiswahili endapo wapendwa na wasomi wetu watapenda tufanye hivyo kwa kutujulisha kupitia maoni yao kwa Mhariri Mkuu.

en-US rocha.chimerah@yahoo.com (Prof. Rocha Chimerah) m.isutsa@pu.ac.ke (Moses R. Isutsa) Tue, 30 Jun 2026 00:00:00 +0300 OJS 3.3.0.11 http://blogs.law.harvard.edu/tech/rss 60 YALIYOMO https://journals.pu.ac.ke/index.php/jss/article/view/8
YALIYOMO
Nafasi ya Kiswahili Katika Sanaa, Michezo na Utamaduni
Kwa Nchi Wanachama Wa Jumuiya Ya Afrika Mashariki
Ahmad Y. Sovu
Ufasiri wa Watoto Wasomaji wa Mhusika Aliye na Ulemavu
Katika Hadithi Teule za Watoto
Mwendwa, S.M., Ngugi, P.M.Y N., na Mutugu, B.N.
Uchanganuzi wa Makosa ya Kimofofonolojia Miongoni Mwa
Wanafunzi Wa Kitachoni Wanapojifunza Kiswahili Kama
Lugha Ya Pili
Makokha, R.M., Ngowa, N. J., Chimerah, R. M., Wallace. S. M.
Uhuru wa Utendaji wa Mashairi ya Harusi ya Waswahili Katika
Miktadha ya Kiisilamu
Mwamzandi, S.Y., Wafula, M., Kandagor, M.
Uwasilishaji wa Ujumbe Kiteknolojia Kwa Kiswahili Katika Vibango
Vya Waganga Wa Kiasili Mjini Eldoret
Njuguna, A.M. na Simala, I.K.
Copyright (c) 2026 Journal of Swahili Studies https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://journals.pu.ac.ke/index.php/jss/article/view/8 Tue, 30 Jun 2026 00:00:00 +0300 Nafasi ya Kiswahili Katika Sanaa, Michezo na Utamaduni Kwa Nchi Wanachama Wa Jumuiya Ya Afrika Mashariki https://journals.pu.ac.ke/index.php/jss/article/view/9
Makala hii inachunguza nafasi ya Kiswahili katika sanaa, michezo na utamaduni katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, ikilenga kubainisha mchango wake katika kuimarisha mshikamano,
utambulisho na
ubunifu. Utafiti umejikita katika Nadharia ya Uchanganuzi Tunduizi Kilongo ya Norman Fairclough
(1995)ya lugha katika muktadha wa kijamii na athari za mitazamo kuhusu lugha hiyo. Data zilikusanywa na kuungwa mkono na Nadharia ya Itikadi za Lugha ya Woolard (1998), ili kufafanua matumizi kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda kupitia usaili na hojaji za mtandaoni, zikihusisha watoataarifa 30 ambapo kila nchi waliteuliwa 6, wakiwamo wahadhiri wa Kiswahili, wasanii, wanamichezo, wanahabari na wataalamu wa lugha. Uchambuzi wa data ulifanywa kwa mkabala wa kimaelezo kwa kuainisha mada kuu na vielelezo halisi vya kauli za washiriki. Matokeo yanaonesha kuwa Tanzania na Kenya zinaongoza katika matumizi ya Kiswahili kwenye sekta husika, ilhali Uganda, Burundi na Rwanda ziko katika viwango vya kati na vya chini. Kiswahili kimethibitishwa kuwa nyenzo muhimu ya mawasiliano ya kisanaa, mshikamano wa michezo na utambulisho wa kikanda. Changamoto zilizobainika ni pamoja na mitazamo hasi, udhaifu wa sera za lugha na uhaba wa wataalamu. Makala inapendekeza kuimarishwa kwa sera za lugha, ufundishaji wa Kiswahili na uwekezaji katika sekta husika kwa maendeleo
Ahmad Y. Sovu Copyright (c) 2026 Journal of Swahili Studies https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://journals.pu.ac.ke/index.php/jss/article/view/9 Tue, 30 Jun 2026 00:00:00 +0300 Ufasiri wa Watoto Wasomaji wa Mhusika Aliye na Ulemavu katika Hadithi Teule za Watoto https://journals.pu.ac.ke/index.php/jss/article/view/11
IKISIRI
Makala hii inaangazia namna watoto wasomaji wanavyofasiri mhusika mtoto aliye na ulemavu katika hadithi teule. Katika tasnia ya fasihi kwa jumla, tafiti zinazohusiana na masuala ya ulemavu zimefanywa na watu wengi. Hata hivyo, tafiti nyingi za awali zimeshughulikia mtindo, wahusika, msigano wa majina ya ulemavu na hata semi na lugha. Aidha, katika fasihi ya watoto, tafiti za awali zimelenga mitazamo ya watoto kwa wenzao walio na ulemavu wa kimwili pekee. Ni katika msingi huu ambapo makala hii imeshughulikia namna watoto wasomaji wanavyofasiri mhusika mtoto aliye na ulemavu katika hadithi teule. Ili kufikia azma hii, mtafiti aliwahoji wanafunzi wa gredi ya kwanza na ya pili kutoka shule za msingi Kaunti ya Kiambu. Makala hii imeongozwa na nadharia ya Udenguzi ya Derrida (1976). Kulingana na nadharia hii, matini ya kifasihi inaweza kufasiriwa kwa zaidi ya njia moja. Data iliyochanganuliwa ilikusanywa maktabani na nyanjani. Maktabani mtafiti alisoma machapisho mbalimbali kama vile makala, tasnifu na vitabu. Nyanjani mtafiti aliwasaili wanafunzi wa gredi ya kwanza na ya pili kutoka shule za msingi Kaunti ya Kiambu. Matokeo ya utafiti yalidhihirisha kuwa watoto watafitiwa walifasiri mhusika aliye na ulemavu kwa njia mbalimbali. Kwa mfano, walimfasiri mhusika aliye na ulemavu kama mhusika wa kuendeleza ushirikiano na mapenzi, mwenye uwezo, mwenye kuonewa huruma/ kudunishwa, anayebaguliwa, shujaa, wa kuigwa, anayenyanyapaliwa, wa kudharauliwa na hata mnyonge. mujibu wa kifungu cha sheria cha NCPWD (2003)
Mwenda S.M, Ngugi P M.Y.N, Mutungu B.B. Copyright (c) 2026 Journal of Swahili Studies https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://journals.pu.ac.ke/index.php/jss/article/view/11 Tue, 30 Jun 2026 00:00:00 +0300 Uchanganuzi wa Makosa ya Kimofofonolojia Miongoni mwa Wanafunzi wa Kitachoni Wanapojifunza Kiswahili kama Lugha ya Pili https://journals.pu.ac.ke/index.php/jss/article/view/12
IKISIRI
Wazungumzi wa lugha ya Kiswahili ambao lugha yao ya kwanza ni Kitachoni hufanya makosa katika
maandishi na matamshi yao kwa lugha ya Kiswahili.Makala haya yamefafanua makosa ya kimofofonolojia
miongoni mwa wanafunzi wanaozungumza Kitachoni wanapojifunza Kiswahili kama lugha yao ya
pili.Wanafunzi lengwa walikuwa wa kiwango cha gredi ya 7 na 8 walio ndani ya mtaala unaojikita katika
misingi ya Umilisi na Utendaji (Competency Based Education (CBE). Lengo mahsusi la kuyafafanua
makosa yaliyofanywa na wanafunzi hawa ni kuweka wazi michakato mahsusi ya kimofofonolojia inayo -
dhihirika na kupendekeza njia za kutatua kitaaluma. Uchunguzi huu uliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi
makosa iliyoasisiwa na Corder (1967) kama mwongozo wa kuchambua makosa yaliyofanywa na
wanafunzi wateule katika gredi ya 7 na 8 na kisha kupendekeza njia mwafaka za kuwaepusha wasomaji
hawa kuyafanya makosa ya kimofofonolojia katika kazi zao za kimaandishi na pia za kimazungumzo.
Kutokana na udurusu wetu maktabani tulibaini kuwa kuna pengo la kiisimu katika ulinganishi wa lugha
ya Kitachoni ambayo ni lugha ya kwanza kwa lugha ya Kiswahili kama lugha ya pili na jambo hili ndilo

Makokha R. M, Ngowa N. J, Chimerah R. M, Wallace S. M. Copyright (c) 2026 Journal of Swahili Studies https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://journals.pu.ac.ke/index.php/jss/article/view/12 Tue, 30 Jun 2026 00:00:00 +0300 Uhuru wa Utendaji wa Mashairi ya Harusi ya Waswahili katika Miktadha ya Kiisilamu https://journals.pu.ac.ke/index.php/jss/article/view/13
IKISIRI

Makala haya yamechunguza uhuru wa utendaji wa mashairi ya harusi ya Waswahili katika miktadha ya
Kiisilamu. Azma yake kuu ni kuchanganua uhuru wa mshairi katika utunzi na utendaji wa mashairi ya
harusi katika jamii ya Waswahili na kutilia manani miktadha ya Kiisilamu. Kupitia mashairi teule;
Wapeni Njia Warembo la Ukhty Dida kutoka Zanzibar na Nataka Kuunda la Bi.Rahma na wenziwe
kutoka Kenya uhuru huu wa utendaji wa mashairi haya uliweza kubainishwa. Mwandishi aliongozwa na
nadharia ya Uhistoria Mpya kuchanganua uhuru wa utendaji katika mashairi haya kwa kuwa nadharia
hii inatilia mkazo umuhimu wa muktadha, historia na utamaduni wa jamii katika utunzi na uhakiki wa
kazi za kifasihi. Utati nyanjani na mtandaoni ulitumika ili kupata data. Shairi la Wapeni njia Warembo
likapatikana kupitia mtandao wa Youtube. Huku shairi la Nataka Kuunda kutoka Kenya likapatikana
baada ya mtati kuzuru maeneo ya Malindi, Kenya akahoji pamoja na kushuhudia utendaji wa shairi hili
Kupitia makala haya tuliweza kubaini kuwa miktadha ya Kiisilamu kamwe haijakuwa kuzuizi katika
uwasilishaji wa mashairi ya harusi ya Waswahili. Watunzi waliweza kutumia uhuru wao sio tu kwenye
utunzi wa mashairi haya, bali pia katika utendaji wake. Makala haya ni muhimu katika uwanja wa fasihi
hasa ushairi kwani yanatoamchango katikamaendeleo ya ushairi na hatua zilizopigwa katika uwasilishaji
wa mashairi ya Waswahili katika miktadha nyeti kama ya Kiisilamu.
Maneno muhimu: uhuru, utendaji, utunzi, miktadha.
Mwamzandi, S.Y., Wafula, M., Kandagor, M. Copyright (c) 2026 Journal of Swahili Studies https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://journals.pu.ac.ke/index.php/jss/article/view/13 Tue, 30 Jun 2026 00:00:00 +0300 Uwasilishaji wa Ujumbe Kiteknolojia kwa Kiswahili katika Vibango vya Waganga wa Kiasili Mjini Eldoret https://journals.pu.ac.ke/index.php/jss/article/view/14
Makala hii inachunguza namna Kiswahili kinavyotumika kuwasilisha ujumbe wa kibiashara katika vibango vya inayosisitiza kuwa maana ya ujumbe hutegemea si maudhui pekee, bali pia mpangilio wa taarifa ndani ya matini.
Data zilikusanywa kwa kupitia, upigaji picha na unukuzi, kisha zikachanganuliwa kwa mkabala wa kimaelezo na kifasiri. Matokeo yanaonyesha kuwa vibango hivi ni miundo ya kimkakati ya mawasiliano inayounganisha lugha, mpangilio wa taarifa, rangi, ukubwa wa maandishi na viashiria vya mawasiliano ya moja kwa moja kama nambari za simu. Kiswahili kilibainika kufanya kazi si kama chombo cha kubeba ujumbe tu, bali kama teknolojia ya kijamii inayorahisisha uelewekaji, kusisitiza vipashio vya maana na kuchochea mwitikio wa haraka wa hadhira.
Aidha, uchanganuzi umeonyesha kuwa muundo wa taarifa hutanguliza vipashio vyenye uzito mkubwa wa kimawasiliano, hivyo kuimarisha mvuto, uelewekaji na ushawishi wa tangazo. Tofauti za kijamii kati ya maeneo ya hadhi ya chini, ya kati na ya juu pia huathiri namna ujumbe unavyopangwa na kufupishwa.Makala inahitimisha kuwa vibango hivi vinapanua mjadala kuhusu mandhari ya lugha, mawasiliano ya biashara na nafasi ya Kiswahili katika uchumi usio rasmi wa mijini katika Afrika ya Mashariki ya sasa kwa namna mpya.
Njuguna S.M., Simala I. K. Copyright (c) 2026 Journal of Swahili Studies https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0 https://journals.pu.ac.ke/index.php/jss/article/view/14 Tue, 30 Jun 2026 00:00:00 +0300