Kauli ya Wahariri
Jarida la Kiswahili (JSS) ni jarida lenye matoleo mawili kwa mwaka. Mipango ya jarida hili ilianza mnamo mwaka wa 2014, japo matoleo ya kwanza yalikuwa mwaka wa 2020.
Jarida hili lilianzishwa kwa minajili ya kukuza na kuendeleza utati na taaluma ya lugha ya Kiswahili kwa kuwapatia watati hawa jukwaa la kuchapisha matokeo ya tatizao. JSS ni jarida ambalo makala yake kuhaririwa na kudurusiwa na wahakiki ili kuhakikisha kwamba uzito wa kiakademia wa makala umedumishwa. Ni matumaini yetu kwamba wasomi wa majarida yetu watanufaika mno kwa elimu iliyomo katika makala ya jarida hili na vile vile ni matumaini yetu kwamba watati wengi wengine
watahamasika kwa kusoma majarida yetu. Iwapo wasomi wa jarida hili wana maoni ya kulifanya liwe bora zaidi, tunawasihi watujulishe kupitia anwani za barua pepe zetu. Tunawatakia usomaji mzuri na wa manufaa wa jarida hili.
Wahariri Wakuu:
Prof. Rocha Chimerah – rocha.chimerah@yahoo.com
Dr. Nancy Ngowa – n.ngowa@pu.ac.ke