Uchanganuzi wa Makosa ya Kimofofonolojia Miongoni mwa Wanafunzi wa Kitachoni Wanapojifunza Kiswahili kama Lugha ya Pili

Authors

  • Makokha R. M
  • Ngowa N. J Pwani University
  • Chimerah R. M Pwani University
  • Wallace S. M. Pwani University

DOI:

https://doi.org/10.2026/jss.v3i1.12

Keywords:

IstilahiMaalum: Lugha ya kwanza, Lugha ya pili, UchanganuziMakosa,Mofofonolojia,Mtalaa wa Umilisi na Utendaji.

Abstract

IKISIRI
Wazungumzi wa lugha ya Kiswahili ambao lugha yao ya kwanza ni Kitachoni hufanya makosa katika
maandishi na matamshi yao kwa lugha ya Kiswahili.Makala haya yamefafanua makosa ya kimofofonolojia
miongoni mwa wanafunzi wanaozungumza Kitachoni wanapojifunza Kiswahili kama lugha yao ya
pili.Wanafunzi lengwa walikuwa wa kiwango cha gredi ya 7 na 8 walio ndani ya mtaala unaojikita katika
misingi ya Umilisi na Utendaji (Competency Based Education (CBE). Lengo mahsusi la kuyafafanua
makosa yaliyofanywa na wanafunzi hawa ni kuweka wazi michakato mahsusi ya kimofofonolojia inayo -
dhihirika na kupendekeza njia za kutatua kitaaluma. Uchunguzi huu uliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi
makosa iliyoasisiwa na Corder (1967) kama mwongozo wa kuchambua makosa yaliyofanywa na
wanafunzi wateule katika gredi ya 7 na 8 na kisha kupendekeza njia mwafaka za kuwaepusha wasomaji
hawa kuyafanya makosa ya kimofofonolojia katika kazi zao za kimaandishi na pia za kimazungumzo.
Kutokana na udurusu wetu maktabani tulibaini kuwa kuna pengo la kiisimu katika ulinganishi wa lugha
ya Kitachoni ambayo ni lugha ya kwanza kwa lugha ya Kiswahili kama lugha ya pili na jambo hili ndilo

References

MAREJELEO

Corder, S. (1967) Error Analysis: Perspective

on the second language acquisition. London:

Longman.

Interlanguage: Oxford University Press.

Habwe, J., and P. Karanja. (2004) Misingi ya

Saru ya Kiswahili. Phoenix Publishers Ltd.,

Nairobi.

Hooper, J. B. (1976). An introduction to natural

g e n e r a t i v e p h o n o logy. Academic Press

Sounds, Sound Changes, and Words. Nairobi:

Focus publishers

Mgullu, R.S. (1999). Mtalaa wa Isimu: Fonetiki,

Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Nairobi:

Longhorn Publishers (K) Ltd.

Downloads

Published

30-06-2026

How to Cite

Makokha, M., Ngowa, N., Chimerah, M., & Wallace, S. (2026). Uchanganuzi wa Makosa ya Kimofofonolojia Miongoni mwa Wanafunzi wa Kitachoni Wanapojifunza Kiswahili kama Lugha ya Pili. Journal of Swahili Studies, 3(1), 31–43. https://doi.org/10.2026/jss.v3i1.12