Uhuru wa Utendaji wa Mashairi ya Harusi ya Waswahili katika Miktadha ya Kiisilamu
DOI:
https://doi.org/10.2026/jss.v3i1.13Keywords:
Maneno muhimu: uhuru, utendaji, utunzi, miktadha.Abstract
IKISIRI
Makala haya yamechunguza uhuru wa utendaji wa mashairi ya harusi ya Waswahili katika miktadha ya
Kiisilamu. Azma yake kuu ni kuchanganua uhuru wa mshairi katika utunzi na utendaji wa mashairi ya
harusi katika jamii ya Waswahili na kutilia manani miktadha ya Kiisilamu. Kupitia mashairi teule;
Wapeni Njia Warembo la Ukhty Dida kutoka Zanzibar na Nataka Kuunda la Bi.Rahma na wenziwe
kutoka Kenya uhuru huu wa utendaji wa mashairi haya uliweza kubainishwa. Mwandishi aliongozwa na
nadharia ya Uhistoria Mpya kuchanganua uhuru wa utendaji katika mashairi haya kwa kuwa nadharia
hii inatilia mkazo umuhimu wa muktadha, historia na utamaduni wa jamii katika utunzi na uhakiki wa
kazi za kifasihi. Utati nyanjani na mtandaoni ulitumika ili kupata data. Shairi la Wapeni njia Warembo
likapatikana kupitia mtandao wa Youtube. Huku shairi la Nataka Kuunda kutoka Kenya likapatikana
baada ya mtati kuzuru maeneo ya Malindi, Kenya akahoji pamoja na kushuhudia utendaji wa shairi hili
Kupitia makala haya tuliweza kubaini kuwa miktadha ya Kiisilamu kamwe haijakuwa kuzuizi katika
uwasilishaji wa mashairi ya harusi ya Waswahili. Watunzi waliweza kutumia uhuru wao sio tu kwenye
utunzi wa mashairi haya, bali pia katika utendaji wake. Makala haya ni muhimu katika uwanja wa fasihi
hasa ushairi kwani yanatoamchango katikamaendeleo ya ushairi na hatua zilizopigwa katika uwasilishaji
wa mashairi ya Waswahili katika miktadha nyeti kama ya Kiisilamu.
Maneno muhimu: uhuru, utendaji, utunzi, miktadha.
References
Abdalla, A. (1973). Sauti ya Dhiki. Oxford University Press. Shairi Halijachapishwa.
Abdallah, R. O. (2024). Nataka Kuunda.
Aqaz Star Maulid (2021). Ukhty Dida Avamiwa na warembo ndani ya Holi kwa Qaswida-Pambe ya Kharusi. Available at https://youtu.be/2aoaKHCTICc?si=8kHB602Vg Tj3ogGD. Imepakuliwa 31/05/2025 saa 10:16.
oucault, M. (1997). The Order of London: Routeledge and Kegan Limited.
Friedrich, P. (1986). The Princes of Naranja: An Essay in Anthrohistorical Method. Austin: University of Texas Press.
Greenblatt, S. (1980). Renaissance Self-Fashioning. Chicago: University of Chicago Press.
Kezilahabi, E. (1974). Kichomi. Heinemann—Educational Books. Knappert, J. (1971). Swahili Islamic Poetry. Brill.
Matundura, E na Wenzake (2017). Mgogoro wa Ushairi wa Kiswahili Miaka Hamsini Baadaye. Jarida la Mwanga wa Lugha.
Mazrui, A.M. (2007). Swahili Ethno-psychology and Cultural Appropriation. Africa World Press.
Mbaabu, I. (1985). Utamaduni wa Waswahili. Kenya Publishing & Book Marketing Co. Ltd., Nairobi.
Mnyapala, M. E. (1970). Nguzo ya Ushairi Kiswahili. East African Literature Bureau.
M- ulokozi, M. Na Kahigi (1979). Kunga za Ushairi na Diwani Yetu. Tanzania Publishing
House. Johari ya Kiswahili: Kidato cha Tatu. Nairobi:
Mumbo, C.K., & Indede, F.N. (2004). Acme Press Ltd.
Munyao, M.K. (2016). Uhuru wa Kishairi katika Utunzi wa Mashairi: Uchanganuzi wa
Sikate Tamaa na Miale ya Uzalendo. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Nasimiyu, M.C. (2016). Athari ya Mazingira ya Kihistoria na Kijamii katika Uwasilishaji wa Maudhui ya Dhifa (E. Kezilahabi). Tasnifu ya Shahada ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Njogu, K., & Chimerah, R. (1999). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu. Nairobi.
Robert, s. (1958). Pambo la Lugha. Oxford University Press.
Sengo, T. S. Y. (1992). Utamaduni wa Kiswahili: Wilaya ya Kusini Unguja. Katika Nordic
Journal of African Studies 1 (1), 53-79.
Shari, N.I. (1988). Tungo Zetu.New Jersey:e Red Sea Press Inc.
Topan, F. (2006). Why Does a Swahili Writer Write? Euphoria, Pain, and Swallowiness.
Research in Literature.
Wamitila, K.W. (2003). Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. Focus Publication Ltd.
Zanzibar One Qaswda (2022).
Ukhty Dida—Wapeni njia warembo (Official video). Available at https://youtu.be/JUS8wGSdY3w?si=
jt6Hipz9iC53Bcks. Imepakuliwa 31/05/2025 saa 10:16.
Downloads
Published
How to Cite
Issue
Section
License
Copyright (c) 2026 Journal of Swahili Studies

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.