Shukrani
Abstract
Ningependa kutoa shukrani za dhati kwa Prof. Mohamed Rajab, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Pwani, kwa kujitolea kwa hali, mali na wakati katika shughuli za jarida hili na kuhudhuria mikutano hapa Pwani na RISSEA ili kuhakikisha kwamba muungano huu wa Chuo Kikuu cha Pwani na RISSEA umefanikiwa pamoja na mradi wetu wa kwanza wa kutoa jarida la Kiswahili. Zaidi ya hayo, Prof. Mohamed Rajab ameahidi kufadhili mradi huu wa jarida kwa miaka mingine mitano hadi uwe na msingi thabiti wa kuweza kujisimamia wenyewe. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (S.W.T) amuneemeshe Prof. Mohamed Rajab neema kubwa kubwa.