Ushairi na Utamaduni
Natija na Mawanda yake katika Tungo za Wamvita
Abstract
Ushairi ni nini? Hili ni swali ambalo lataka uyakinifu kulijibu. Twasema hivyo kwa sababu kuna tetesi za wanaojiita wanamapinduzi wa ushairi; nao wanaodai kuwa; “Ushairi ni mtiririko wa mawazo yenye kuilimisha au kupumbaza jamii na ati hapana lazima ya kufuata arudhi”. Yaani mawazo hayo si lazima yawe yatafuata kanuni za kuchunga mizani na vina. Sisi tuitwao wana hafidhina twasema “La! La! Hashaa wa kalla!” Ushairi si kupanga misitari ya maneno au kuandika barua. Mimi naona watu hao kama hawawezi kutunga mashairi ni afadhali waandike riwaya au tamthilia kueleza mawazo yao. Kwani mashairi ya kale yalikuwa na vina ijapoku- wa mengineyo hayakuwa na sharti la kuandamisha mizani.