Miongo Mitano ya Fasihi ya Kiswahili nchini Tanzania: Maendeleo, Changamoto na Mustakabali Wake

Miongo Mitano ya Fasihi ya Kiswahili nchini Tanzania

Maendeleo, Changamoto na Mustakabali Wake

Authors

  • Alex Umbima Kevogo Idara ya Lugha, Isimu na Fasihi, St Agostino University, Tanzania

Abstract

Tanzania inaposherehekea miaka hamsini ya uhuru, makala haya yamechunguza historia na maendeleo ya fasihi andishi ya Kiswahili ya Tanzania ndani ya kipindi cha miongo mitano baada- ya uhuru. Msisitizo maalumu umekitwa kwenye mikondo ifuatayo inayojitokeza: Kuibuka kwa fasihi inayoihakiki jami; Kuibuka kwa fasihi ya kimajaribi; Chimbuko la fasihi pendwa; Kuzuka kwa fasihi ya kizalendo; Athari za utandawazi na tafsiri za kazi za fasihi zenye asili ya kigeni. Haya yote yamezingatia mkabala wa kihistoria unaotathmini maendeleo ya kijamii, kisiasa, kitamaduni na kiuchumi nchini Tanzania miaka hamsini baada ya uhuru.

Downloads

Published

2022-09-12

Issue

Section

Articles
Loading...