Nafasi ya Kiswahili Katika Sanaa, Michezo na Utamaduni Kwa Nchi Wanachama Wa Jumuiya Ya Afrika Mashariki

Authors

  • Ahmad Y. Sovu

DOI:

https://doi.org/10.2026/jss.v3i1.9

Abstract

Makala hii inachunguza nafasi ya Kiswahili katika sanaa, michezo na utamaduni katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, ikilenga kubainisha mchango wake katika kuimarisha mshikamano,
utambulisho na
ubunifu. Utafiti umejikita katika Nadharia ya Uchanganuzi Tunduizi Kilongo ya Norman Fairclough
(1995)ya lugha katika muktadha wa kijamii na athari za mitazamo kuhusu lugha hiyo. Data zilikusanywa na kuungwa mkono na Nadharia ya Itikadi za Lugha ya Woolard (1998), ili kufafanua matumizi kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda kupitia usaili na hojaji za mtandaoni, zikihusisha watoataarifa 30 ambapo kila nchi waliteuliwa 6, wakiwamo wahadhiri wa Kiswahili, wasanii, wanamichezo, wanahabari na wataalamu wa lugha. Uchambuzi wa data ulifanywa kwa mkabala wa kimaelezo kwa kuainisha mada kuu na vielelezo halisi vya kauli za washiriki. Matokeo yanaonesha kuwa Tanzania na Kenya zinaongoza katika matumizi ya Kiswahili kwenye sekta husika, ilhali Uganda, Burundi na Rwanda ziko katika viwango vya kati na vya chini. Kiswahili kimethibitishwa kuwa nyenzo muhimu ya mawasiliano ya kisanaa, mshikamano wa michezo na utambulisho wa kikanda. Changamoto zilizobainika ni pamoja na mitazamo hasi, udhaifu wa sera za lugha na uhaba wa wataalamu. Makala inapendekeza kuimarishwa kwa sera za lugha, ufundishaji wa Kiswahili na uwekezaji katika sekta husika kwa maendeleo

References

Batibo, H. M. (2005). Language Decline and Death in Africa: Causes, Consequences, and Challenges. Multilingual Matters.

Blommaert, J. (2014). State Ideology and Language in Tanzania: Second and Revised Edition. Edinburgh University Press.

EAKC (2019). Capacity Assessment of the Development and Use of Kiswahili in the EAC. Arusha: EAC.

Fairclough, N. (1995). Critical Discourse Analysis: The Critical Study of Language. Longman.

Karanja, L. W. (2003). Language in Education and Language Policy in East Africa. Oxford: African Books Collective.

Katoke, I. (2004). History of East Africa. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House.

Kiango, J. G. (2015). Kiswahili katika Ukanda wa Afrika Mashariki: Mwelekeo wa Kijamii na Kiutamaduni. Nairobi: Longhorn Publishers.

Legère, K. (2006). Promoting the Use of African Languages in Education: A Case of Kiswahili. In: UNESCO Conference Papers on Multilingualism. Power of Babel: Language and Governance in the African Experience. University of Chicago Press.

Mulokozi, M. M. (1999). Kiswahili na Maendeleo ya Afrika. Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI).

Ntabo, R. (2017). “Kiswahili katika Maendeleo ya Jamii ya Afrika Mashariki." Jarida la Kiswahili, 83(2), 45-61.hili in East Africa: A Historical Perspective”.TUKI Journal of African Languages, Vol. 5.

Silverstein, M. (1979). “Language Structure and Session on Linguistic Units and Levels." van Dijk, T. A. (2001). Discourse and Power. Palgrave Macmillan.

Woolard, K. (1998). “Language Ideology as a Field of Inquiry." Language Ideologies: Practice MAREJELEO and Theory, 3-47.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2025), Dira ya Taifa 2050

(https://nasseryouthmovement.net/sw/Kiswahili-

Uchumi-Afrika-Mashariki-BAKITA). Imesomwa tarehe 19, Mei, 2026.

Downloads

Published

30-06-2026

How to Cite

Sovu, A. (2026). Nafasi ya Kiswahili Katika Sanaa, Michezo na Utamaduni Kwa Nchi Wanachama Wa Jumuiya Ya Afrika Mashariki. Journal of Swahili Studies, 3(1), 6–16. https://doi.org/10.2026/jss.v3i1.9